NGUVU YA NAFASI
YA MWISHO.
Kama utafanya jambo kiasi-
kwamba hautapata tena-
nafasi nyingine kulifanya,
hakika utakuwa mshindi ---
wa jambo hilo.
Linapokuja swala la nguvu ya nafasi ya mwisho -kila mtu anaguswa kwa aina ya
kipekee kabisa -kwani kila mmojawetu kwa
nafasi yake alishawahi kupitia katika nafasi
ambayo ilikuwa ya mwisho kabisa kwenye
kuliteda jambo hilo.
Aidha kwa kujua au kutojua ,lakini hata wewe mwenyewe ulishapita kwenye nafasi fulani katika maisha yako na ukaona kama vile ni nafasi ya mwisho ya kutenda jambo hilo.
Mfano wa nafasi za mwisho tulizozipitia na tutakazozipitia katika maisha yetu ni kama vile:- siku ya mtihani wa mwisho kuhitimu elimu fulani,siku ya mashindano ya mchezo fulani, n.k.
Unaionaje nguvu/msukumo ambao huwa upo ndani yako ikiwa ni nafasi ya mwisho ya kutenda jambo hilo.na hautapata tena nafasi nyingine kulitenda jambo hilo maishani mwako .
Hapa ndo utaona upekee wa binadamu, kila mtu huwa yupo tofauti akiwa na utulivu huku akiamini uwezo wake wa ndani na anachokijua.
Lakini siri uliokuwa haufahamu katika siku ya nafasi ya mwisho ni kwamba:-kuna nguvu ya aina ya kiutofauti ambayo huwa ndani ya mtu -humsaidia mtu kupambana
kadri awezavyo ili kushida.
Ndugu msomaji na mfuatiliaji wa wezamtima@.. -- nguvu hii ya nafasi ya mwisho inahitajika kutumika hata katika maisha ya kawaida ya kusaka mafanikio.
Amini nakuhakikishia kuwa kiu chako cha kufanikiwa kutimia --kinahitaji nguvu ya aina yake ya kujitoa kutafuata hayo mafanikio kiasi kwamba hautapata tena nafasi nyingine .
Kama utazamishwa ndani ya maji kwa dakika kadhaa hivi,na ukawa na kiu kubwa ya kutaka kuibuka na kuvuta hewa, kuhema,kiu hivyo ni sawa na nguvu ya nafasi ya mwisho.kama ulivyokuwa unaisaka nafasi ya kupata hewa/kuhema katika maji --kiu hivyo itumie na kutafuta mafanikio.
SIFA ZA NGUVU YA NAFASI
YA MWISHO.
1. USHINDI.
Mtu akipewa nafasi ya mwisho huhesabu kushinda ,huamini sana akili na uwezo wake.
2. UMAKINI.
Umakini huwa ni wa hali ya juu kuliko kawaida ya siku zote ,kuhakikisha kuwa hakuna kitu cha kukosea.
3. UWEZO.
Uwezo wa mtu wa ndani humfariji mtu na kumhakikishia kuwa anaweza kushinda.
4. UHAKIKA.
Imani isiyo ya kawaida huwa iko na mtu anapokuwa katika kuitumikia nafasi ya mwisho kufanya jambo.
5. UZINGATIVU.
Kama ni kanuni atazingatia ,yaani kila kitendo anachotenda atazingatia maelezo au kanuni maalumu.
6. UVUMILIVU.
Uvumilivu humjia kwa kiwango kisicho ukomo ,hawezi- choka kabla ya kuhitimisha jambo.
7. JITIHADA.
Liwalo na liwe lakini juhudi zote huziweka mtu katika siku ya nafasi ya mwisho.
8. UTII.
Hukubaliana na kila utaratibu na kuwa chini ya sheria ilimladi tu afanye kwa ufanisi jambo hilo.
9. UTEKELEZAJI.
Huwa hana mda mwingine tena wa kutekeleza jambo hilo ,hivyo fikra zote hufikiri na kutekeleza jambo hilo.
Ndugu yangu napenda utambue kuwa maisha ya mafanikio sio kazi rahisi ,hivyo tunahitaji sana nguvu hii ya nafasi ya mwisho kutimiza malengo ya ndoto zetu.
-Leo amua kushinda kila changamoto,
Ili ufikie kilele cha ndoto yako.
= Joeli Nanauka.
Ona kama ndo umepewa nafasi nyingine ya mwisho kutafuta mafanikio ya ndoto zako. Badili fikra ili kesho yako iwe nzuri .
I am who I am to day because of -
the decision i made yesterday.
=Eleanor Rooselvelt.
SABABU ZINAZOWAFELISHA WATU
WAKIWA KATIKA NAFASI YA MWISHO
YA KUTEKELEZA JAMBO
- Umakini mdogo wakuitumia nguvu ya nafasi ya mwisho
- Wasiwasi unaotokana na upekee wa nafasi hii.
- Kutokujiamini na kuogopa ushindani.
- Kuwa na huzuni -iliyosababishwa na hali za kimaisha ,:- msiba ,nk.
- Maandalizi madogo ukilinganisha na ukubwa wa nafasi hiyo ya mwisho.
Natumai tunaenda sambamba mwanaharakati wangu,uliye na fikra za kipekee kabisa juu maisha .najitahidi kufafanua bila kukuchosha ili ujue unahitaji hamasa,upeo na nguvu kiasi gani kufika unakotaka kwenda.
Sina la ziada nakuachia utajiri wa hiyo nguvu ya nafasi ya mwisho ,nadhani uhalisia wa maisha yako unaufahamu we we mwenyewe zaidi kuliko mimi. Hii ni nafasi nyingine ya mwisho uliopewa maishani mwako ,sidhani kama utaitumia vibaya.
Anthony Elia Mwaka
Mwandishi
Mjasiriamali
Muigizaji.
Tel.no. +255659594226
+255738651846
wezamtima@gmail.com
www.wezamtima.com.
Born-Dodoma, live-Dar es salaam.
Kina cha fikra hakina ukomo.
No comments:
Post a Comment