KATA UTEPE
MBELE KWEUPE
Unavyoyatafsiri maisha -ndivyo
utakavyo yaishi. Lakini namna
unavyofikiria kuhusu maisha,
Ndivyo utakavyo-tenda.
Na matendo yako -ndio--
Yatakuwa maisha yako.
Ebu nijaribu kukurudisha nyuma-------
miaka kumi ya maisha yako iliyopita ,kama
nigelikutana na wewe ningelikuuliza swali-hili:- "Hamisi --hivi miaka kumi ijayo utakuwa haumiliki hata ka-gari ka kutemb-elea?
Kwa uharaka na uhakika ungenijibu kuwa
miaka kumi ijayo ungekuwa unamiliki gari
Nzuri la kisasa, nyumba na mafanikio mengi tu ya ndoto zako.
Sasa mda huu mikaka kumi imeshakwisha
na nimekuja tayari tuone majibu uliyonijib-
u yametimia? Majibu unayo wewe mweny--
ewe kiukweli.
Kama majibu uliyonihakikishia kipindi kile
miaka kumi iliyopita yametimia unastahili
Pongezi lakini kama hakuna jipya lililojitok-
eza na maisha unayaona afadhali ya jana---,
Unahitajika kukata UTEPE, --habari njema
mbele ni KWEUPE.
Swali nalokuachia ktk siku ya Leo ni kwam-
ba:- unadhani miaka kumi ijayo jamii yako
na dunia kwa ujumla itajivunia nini kutoka
kwako?watu watakuhitaji kwa kiwango gan
i kutatua shida zao? .Kiukweli unahitajika
kukata utepe, ila habari njema mbele ni -----
kweupe.
UTEPE NI NINI?
Utepe ni ugwe(kamba) wa kitambaa au
nguo. Tafsiri hii ni kwa mujibu wa kamusi
sanifu ya kiwahili. Kisanaa jinsi nilivyolitu--
mia neno utepe -ni ukanda kati yako na ------
kule unakoelekea(mafanikio).
Kukata utepe maana yake ni ni namna gani upambane na changamoto zinazokuzonga
ktk mambo hususani kama yafuatavyo:-
- Ktk unachokifanya .
Inawezekana kuna changamoto kadha wa--
kadha ktk kazi yako ,ktk chochote unachokifanya siku hizi, ila tambua kuwa kila mtu aliyewahi kufanya unachofanya ---
alikumbana na changamoto mbali-mbali
kama unazopitia wewe au nyingi hata wew
e haujazipitia.
Mara nyingi watu huona kama ni mikosi
kupitia ktk changamoto ,ila tu nikwambie
kuwa sio mikosi bali ndio utaratibu wa ----maisha ,changamoto zipo duniani na kila
mtu atazipitia ,--lakini mchakato wa kutatua changamoto niendelevu hadi mwaisho wa uhai wetu duniani.
Leo kata utepe tafuta suluhisho la changa---
moto zinazokusumbua na sio kulalamika
na kukata tamaa.
- Ktk unachotamani kukifanya.
Kuna wakati huwa unaogopa kutoa maamuzi ya kufanya kitu cha ndoto zako
au biashara fulani au kitu kingine.kata utepe anza kufanya hakuna muda au wakat
i ambao utakuwa sahihi kufanya ,anza sasa.
- Ktk kufilisika kwako.
Kufilisika ni kutokupata matokeo chanya kwa kileulichowekeza ,au kuplomoka kutoma juu ulipofikia hadi chini kiasi kwamba unaanze upya tena kwenda juu.
Kama hali hiyo imekukuta ,unachotakiwa kufanya ni kukubali kuwa umefilisika,pili,
kukata utepe na kuanza safari upya -kwani
una uzoefu wa hali ya juu.
- Ktk woga.
Woga unawasumbua watu wengi sana maishani, ni kweli kuna vingi vya dunia vinatisha -kama vile:- magonjwa, njaa, umaskini, vita,nk. Lakini tu nikwambie ndugu msomaji kuwa, kuishi kwa kuogopa viogovya vyote vya dunia --ni maisha mabaya zaidi kuliko unavyoviogopa.
Kata utepe ishi ukiwa huru kuanzia akilini
,moyoni na mwilini,kwani mbele kweupe.
- Ktk maumivu.
Kwakuwa changamoto zitakujia maishani
kwahiyo tambua kuwa kuna wakati utapita
Ktk maumivu, aidha usababishiwe au uyasababishe mwenyewe.
Kata utepe ,mbele ni kweupe ,maumivu uliyonayo ni ya muda mfupi tu .
- Ktk uzingativu.
Kitu kinachokwamisha mafanikio ya watu
walio wengi ni:- kutokuwa na uzingativu
ktk jambo moja ,bali wanajaribu kufanya kila kitu,kila fursa.
Kata utepe, wekeza nguvu na akili zako ktk kitu kimoja cha ndoto zako ,unachokitenda
Kutoka moyoni, utaona mbele ni kweupe.
DHUMUNI KUU LA KUKATA UTEPE KTK
MAKALA HAYA.
Dhumuni la makala haya ni kukutaka uelewe tafsiri halisi ya neno Maisha, na uchukue hatua za haraka kuweza kubadili fikra ili kufikia ndoto zako au kule
unakoelekea.
MAISHA NI NINI?
Maisha ni muda wa uhai wa kiumbe. kwa mujibu wa tafsiri ya kamusi ya kiswahil sanifu.
Kumbe kila mtu ana maisha bila upendeleo
wowote ,tena maisha mazuri kabisa . kila binadamu kaubwa na Mungu kwa kusudi
maalumu aje duniani aishi muda maalumu
, akamilishe jukumu maalumu.
Maisha hayahitaji uwe na wasiwasi kwa
kila jambo ,ila yanahitaji utulize uwezo uliojaliwa,ulioumbwa nao na Mungu, uwezo huo ukusaidie ufike unapopataka kulingana na kusudi la Mungu na mpangilio wa ndoto zako.
NAMNA YA KUKATA UTEPE NA KUONA
MBELE KULIVYO KWEUPE.
1. Kubadiri fikra.
Kila mabdailiko huanzia kichwani ktk fikra.
Kubali kuwa na fikra tofauti hasa kutoka kwa watu mbali-mbali ,kutana na watu ,soma historia za maisha yao, huzuria semina mbali-mbali za hamasa na mafanikio.nk.
2.jua kusudi .
Tambua upo duniani kwa kusudi gani ,na una ndoto gani kutimilisha kusudi hill.
3.tafsiri chanya .
Tafsiri chanya ndio mafanikio yenyewe ktk maisha ,matatizo yote hutatuliwa kwa mawazo chanya tu.
4. Maono.
Ielekeze akili yako kwa tafsiri chanya kule kunako matamanio ya mafanikio yako.
5. Ndoto.
Usiishi ilimladi tu siku ziende ,ukishajua kusudi lako ,panga ndoto zako na uanze kuzitekeleza.
6. Mwelekeo.
Songa mbele kata utepe kueleke ndoto zako ziliko ,mbele kweupe ,changanua changamoto.
7. Jinsi ya kufika huko.
Umeshauona mwelekeo ,sasa utafikaje huko ,usijiulize sana ,anza safari tepe zitakuwa nyingi njiani ,kata moja moja ila habari njema ni kwamba--mbele ni kweupe.
Najivunia wewe unaefuatilia wezamtima@.., endelea kujionea majabu ya mabadiliko ya kimafanikio maishani mwako .
By,Anthony Elia Mwaka.
Mwandishi
Muigizaji
Mujasiliamal.
Tel. +255659594226
+255738651846
Wezamtima@gmail.com
Website= www.wezamtima.com
Dodoma -Tanzania.
Kina cha fikra haikina ukomo.
No comments:
Post a Comment