UBORA NA UFANISI.
Mafanikio ni matokeo ya ubora na
ufanisi kwa unachokitenda kwa
kila siku bila kujali ugumu wa
mazingira au maslahi binafsi.
Nianze kwa kukuhusisha na simlizi ya kusisimua ya kijana mmoja aitwaye Lostam Magana.
Lostam alikuwa akifanaya kazi ktk hali ngumu ya manyanyaso ktk mgahawa mmoja huko Temeke jijini Dar es laam.
Lostam alipata kazi hiyo baada ya kuteseka sana na hali ya utoto wa mtaani kwa zaidi ya mika kumi tangu mama yake afariki dunia na kumuacha na umri wa miaka nane huku akiachwa hana baba kwani mama yake alikuwa mwathilika wa
madawa ya kulevya (teja) --hivyo hakujua wala hakujali aliupata wapi ujauzito wa Lostam.
Lostam alilelewa mtaani pamoja na watoto wenzake wa mtaani ktk mazingira yasiyoelezeka (magumu) hadi alipokua na kupata kazi ktk mgahawa fulani huko Temeke jijini Dar es salaam.
Licha ya Lostam kuona kama ahueni ya maisha mgahawani kuliko ya mtaani -lakini
bado alikuwa kakumbwa na zongo la manyanyaso na ugumu wa maisha.
Alitumikishwa kazi kupita kiasi ,yaani alala saa sita usiku na kuamka saa tisa kwaajiri ya kazi kwa ujira wa 2500Tsh kwa siku.
Lostam hakukata tamaa aliendelea kujitu-
ma na kuonesha ubora na ufanisi wake ktk kazi ,alitii na kufuata masharti yote ya msimamizi wa mgahawa huo licha ya kupitia ktk mazingira magumu.
Siku moja mmiliki(boss) wa mgahawa huo alitembelea mgahawani kwake ,-ilikuwa ni miezi saba baada ya Lostam kuajiriwa pale mgahawani.
Siku hiyo Lostam aliamlishwa na msimamizi wa mgahawa huo kuwa amhudumie boss wao , Lostam alitii kama ilivyo kawaida yake na ubora wake na ufanisi akamhudumia boss.
Baadae akaitwa na boss na kuambiwa kuwa tangu siku hiyo ndio mwisho wa kufanya kazi ktk mgahawa ule.kwani boss alivutiwa na ufanisi wake ktk kazi na akaamua kumpeleka moja ya hoteli zake kubwa kulingana na ubora na ufanisi wake.
Tangu siku ile Lostam akaandika ukurasa mpya wa maisha yake - hadi navyoandika makala haya sasahivi -Lostam ni meneja msaidizi wa hoteli zote zinazomilikiwa na huyo boss.
UBORA NA UFANISI NI NINI?
Labda unajiuliza maana na tafsiri ya maneno haya mawili yanayotikisa kurasa za makala haya.
UBORA ni thamani ya kitu au hali ya upekee isiyofananishwa na ya kitu kingine.
UFANISI ni ya kupatikana kwa mafanikio au usitawi.
Kwahiyo maana ya ubora na ufanisi ni thamani ya usitawi wa mafanikio fulani .
Thamani hii ya usitawi wa mafanikio fulani hujengwa na matendo ya mtu ya kila siku. Je huwa unafanya mambo kwa kuangalia maslahi tu? au kwa kuangalia Leo tu?.
Unapofanya vizuri kwa viwango vya juu bila kujali ugumu wa mazingira au maslahi unajiwekeea utayari wa mafanikio mbeleni ,amini nakwambia unachokitoa ni lazima uje kukipokea -hata kama kitachelewa .
Nimnukuu mhamasishaji wa kujitambua na mwandishi nguli wa vitabu nnchini Tanzania ,-alisema:-
1. "Wengi wetu tunataka utukufu,laki--
ni hatutaki safari ya kuelekea utukufu huo".
=Eric Shigongo.
2. " bahati hujengwa na binadamu mwenyewe ,unapofanya kazi kwa nguvu zaidi ndivyo unavyopata bahati zaidi ya kufanikiwa".
=Eric Shigongo.
Chochote unachofanya Fanya kwa ubora na ufanisi wako wote utakuwa unajiweka kwenye bahati ya kufanikiwa, mafanikio yoyote yale ni matokeo ya nguvu ya ubora na ufanisi wa matendo yaliyopita.
MAMBO YA KUFANYA ILI UWE BORA NA MFANISI
1. Fikiri kabla ya kutenda.
Kumbuka matendo unayoyatenda ndio maisha yako ya kesho, tathimini na uangalie faida ya kesho ya matendo hayo.
2. Jione unaweza hata pasipo na njia.
Uwezo wako haushindwi kitu ,fikra hazina ukomo ,chochote unachotaka kimo.
3. Waza chanya.
Usiruhusu wala kuangalia yale mambo hasi ,bali zingatia mambo chanya bora ya kukujenga ,kwani matatizo yote hutatuliwa kwa fikra chanya.
4. Kuwa wa viwango.
Yaani sio mtu wa kawaida wala haufananishwi na yeyote duniani ,na kila unachokifanya unafanya kwa ustadi wa hali ya juu sana,haijalishi kitu hicho kidogo au kikubwa.
5. Uwe wa pekee.
Wewe ni wewe tu ,utambulisho wako ni namna ulivyo bora na mfanisi ktk matendo yako yote .
6. Jitoe .
Kujitoa ni hali ya kung'ang'ania jambo na kuamini litatokea ,na kufanya hadi upate matokeo uliyoyakusudia.
7. Jitathimini.
Wote walio bora na wafanisi hujitathimini na kujipongeza kwa mazuri waliyofanya ,kuupa mwili na akili ushindi wa kufanya na mambo mengine kwa ubora na ufanisi.
Kujitathimini pia hugundua makosa na kasoro zako na kujilekebisha.
8. Jifunze.
Kujifunza ni jambo endelevu ,usipojifunza kila kukicha - utaachwa mbali sana na dunia hii inayoenda kasi na ushindani wa maarifa.
9. Amini na uifuatilie imani yako.
Isiwe tu kuwa we we ni mtu wa imani fulani --lakini ukawa hauijui imani yako - ni hasara. Mtoto yatima hujiona ni mpweke na asiye na usalama kuliko yule mwenye wazazi. Ukijifungamanisha ktk imani yako utajiona usiyeteteleka .
10. Tekeleza.
Hata uendele kujifunza vipi ,kama hauchukui hatua za uthubutu na utekelezaji hauwezi pokea mabadiliko ktk maisha yako.
Sina la ziada ,nashukuru kuwa nawe na endelea kunifuatilia mpaka maisha yaimalike ktk mafanikio.
By, Anthony Elia Mwaka.
Mwandishi
Mjasiriamali
Muigizaji.
Tel. +255659594226
+255738651846
Wezamtima@gmail.com
Websites, www.wezamtima.com
Dar es salaam--Tanzania
Kina cha fikra hakina ukomo.
No comments:
Post a Comment