Wezamtima@...

Dar es salaam, Dodoma, Tanzania

Saturday, October 19, 2019

UFAHARI WA KUJITAMBUA.

               UFAHARI WA KUJITAMBUA.

     Umasikini wa kiwango cha juu kabisa-
     ni ule wa kutokuijua thamani   --yako-
                      Na upekee wako.


          Ufahari wa kujitambua ni nini?,najua-
unazijua fahari nyingi sana za hapa dunian
i ,kama :- majumba, magari, ndege, na mafanikio mengine makubwa tu -nayo Yote
ni fahari za hapa duniani.

          Lakini leo ni siku ya kipekee mno ili--
tujifunze huu ufahari wa kujitabua ni ufahaari wa aina gani.

Ufahari wa kujitambua ni sentensi iliyojengwa kwa maneno makuu mawili nayo ni  --ufahari (fahari)
                --kujitambua (tambua).

  • Neno (fahari) maana yake ni "ukuu/utukufu---jambo au kitu cha sifa cha kujivunia kwa watu". 

Na neno (tambua) maana yake ni "kukumbuka au kujua  uasilia wa kitu au jambo fulani". Hii ni kwa mujibu wa tafsiri ya kamusi ya kiswahili sanifu.

            Kwahiyo kwa ujumla maana ya sentensi ufahari wa kujitambua ni kujua----
Utukufu /ukuu /thamani/upekee --ambao kiasilia uliumbwa nao na haufanani na wa
mtu yeyote yule.

Kujitambua Sio jambo la kawaida kama unavyodhani,  jua kuwa -kinachotutofautisha wanadamu -mmoja na mwingine ni namna tunavyojitambua.

Wale wanaojitambua zaidi ndio wanaofanikiwa zaidi maishani, na wasio jitambua -utashangaa Mpaka wanakuwa wazee kabisa lakini hawajafanikiwa na hawana hata fahari yoyote ya kujivunia.

   Njia yakinifu za kujitambua mwenyewe
   na kuanza kunufaika na fahari hii ya ku-
   jitambua, kama fahari yako ya kwanza---
                  ya Muhimu duniani.

1. Asili yako.
 Ijue asili yako, umezaliwa wapi, mna utamaduni na desturi gani, ni nini vya thamani mnavyojivunia kwenu. Kumbuka wanaofanikiwa duniani ni wale wanaofanikiwa kuutangaza utamaduni. Wao na kuuuza.

2. Upeo na vipaji vyako.
Usijidharau na kujiona huwezi kwa namna ulivyo, Mungu kakuumba na uwezo wa kipekee ambao haufanani na wa mtu yeyo-
te yule duniani. Tambua vipaji vyako na Fanya unavyoona inafaa bila kuangalia watu watasemaje --ilimladi tu usivunje maadili na sheria za nchi.

3. Kujifunza.
Kujifunza ni jambo la msingi na endelevu
Katika kukuza na kuendeleza kujitambua kwa mtu. -- ukijifunza kwa kila mtu unaeonana nae, kutananae --basi wewe hautakosea,.
                  --- Jifunze kwa kusoma vitabu --kama unavyofanya muda  huu, Kuna nguvu ya pekee sana katika kujisomea.
                 ---- Jifunze kwa kusikiliza na kutazama pia vitendo mbalimbali vya watu.

4. Ishi upeo wako.
Kuiiga ni jambo zuri tu -kama unaiga chenye manufaa, usiishi maisha ya kuigiza tu kila kitu, kuwa na maisha asilia ya kwako peke yako kwa maana ndicho kitakachokuwa utambulishao wako. Na ita-
kuwa fahari kwako Kama watu wataiga upekee wako.

5. Tekeleza majukumu yako.
Usiishi kwa kushindana na watu, ama usitafute mafanikio ili umpite fulani, hapana.
Fanya unachofanya ili kutimiza majukumu ya maamuzi yako uliyoyatoa. kwa ujumla shindana na majukumu yako.


         Kamwe hautalalamika hata siku moja kuwa Wewe ni maskini kama tu utakuwa umejitambua, fahari ya kujitambua ndio fahari ya kwanza ambayo mtu anatakiwa awe anaifahamu. Ebu anza na kuitafuta fahari Hiyo fahari nyingine zitakuja zenyewe.


Wezamtima@..tumejidhatiti kwa dhati kabisa kuhakikisha watu wengi wanajitambua na kuendana na dunia ya sasa, inayoenda kasi ikiwa imejawa na ushindani wa maarifa.

Karibu sana utaendelea kunufaika na machapisho mengine ya tija ya kutukomboa maishani --kizuri kula na nduguyo -usiwe mchoyo washirikishe na wengine wapate maarifa Haya.


  Anthony Elia Mwaka


Mwandishi,mjasiliamali,muigizaji.


Tel:- +255659594226,
         +255738651846,
         +255687466963.

www.wezamtima.comwezamtima@gmail.com

www.wezamtima.com


Nguvu ya fikra haina ukomo.



No comments:

Post a Comment

UPANA WA ELIMU.

                        UPANA WA ELIMU.            Kila swali katika dunia hii,           linaweza kujibiwa kwa majibu-            ...