RAFIKI WA MAFANIKIO NI TABIA.
Haijalishi ni matokeo chanya au
hasi --yote hutokana na tabia za
kila siku zinazotendwa na mtu .
Uumbaji wake Mungu kwa mwan--
adamu ulibuniwa kwa mfumo wa ufanisi ---
wa kipekee sana. Yaani namna mfumo mn--
zima wa mwili unavyofanya kazi kwa mpa-
ngilio unaojiendesha wenyewe.
Wataalam na watafiti wa masuala ya mifumo ya mwili wa mwanadamu wanasema kuwa - tabia ya mtu inayoanzia
ndani hutoka nje na kumpa vitendo,vitendo
hivyo hunukuliwa na mwili,ubongo na sehem za hisia ,hutengeneza muunganiko wa ushirikiono ktk kile kitendo . Nacho huwa ni tabia ya kila siku.
TABIA.Tabia ni nini?
Tabia ni mazoea yanayotokana na kurudia
rudia hali,mwenendo au matendo.
MAFANIKIO.
Mafanikio ni nini!?
Mafanikio ni matokeo mazuri ya jambo
lililokusudiwa au halikukusudiwa.
Kwahiyo tunaposema rafiki wa mafanikio ni tabia maana yake ni :- tabia
zako za kila siku ndizo zitaleta matokeo ,
ambayo ndio mafanikio yako.
Ila inabidi ufahamu kuwa ,kama una tabia
ambazo si rafiki wa mafanikio yako ,ujue
kuwa hutafanikisha unachokitaka.
Kanuni iko hivi:-
- Mtu(m)
- Tabia(t)
- Matokeo(mt)
- Mafanikio (mf).
M+t=mt
Mt+t=mf(chanya au hasi)
Kwa hiyo kama umenielewa vema mpenzi
msomaji --usiendelee kulalamika au kulaumu watu juu ya mafanikio yako, bali
amua kujenga tabia ambazo zitakuwa rafiki
na mafanikio yako ,na uzitende kilazoea kw
a kila siku.
NJIA ZA KUJENGA TABIA RAFIKI NA
MAFANIKIO YAKO.
1. Kuwa na fikra chanya.
Yachukulie maisha yako ni wajibu wako na
wew ndo mwenye kuwajibika kwa kiwang-
o chote. Fikra chanya hujenga picha nzuri
na matokeo mazuri --kwani -utakachokifik-
iri na kukitenda ndicho mafanikio yako.
2. Malengo na malengo.
Bila mpango au lengo -hakuna unachokifanya.
Jiwekee malengo yako ya ndoto zako
Kuelekea kule unakotaka kufika.
3. Kiu ya utekelezaji.
Jitoe kwa dhati kutekeleza unayojipangia,
maisha unayotaka uishi .
4. Bajeti.
Watu wengi wanaishi kama kuku ilimladi
liende ,hawatako kujichosha,akipata hela
anatumia tu bila na utaratibu maalumu.
Hakikisha unajua kila sh yako inatumikaje
maana usije ukatuletea hadithi za usemi--
huu:- (napata tu hela ila sijui zinakoenda).
5. Takwimu.
Kuwa na kumbukumbu ya mambo yako yote juu ya maisha yako.
6. Mtandao wa watu.
Hakuna mafanikio bila watu, jifunze namna ya kuishi na watu vema ili upate
wa kukushika mkono huko uendako.
7. Uwekezaji.
Ni njia ya kipekee sana wanayoitumia watu wengi wanaofanikiwa .
8. Uthubutu.
Hakuna muoga aliyefanikiwa ,huu ni ulim--
wengu wa majasiri tu, umakini ni kitu cha
msingi zaidi, Fanya kitu tuone.
9. Ratiba.
Yaandike mambo mhimu ya kufanya kesho
leo kabla ya kulala --na kesho uyatimize kama ulivyopanga katka ratiba yako.
Tafakar siku yako na ujipongeze na kujilekebisha unapoona umeenda sivyo.
10.Utekelezaji.
Tekeleza yote unayoyapanga maishani mw-
ako kwa maana ndio ushindi wako wa mafanikio.
Ndugu msomaji -maisha ni kupanga
na kuchagua kipi kiwe kipaumbele.naamin
kila mtu huwa ana hitaji la mafanikio ili
aishi kwa fulaha, lakini itakuwa bora zaidi
kama utaanza na kuitafuta furaha halafu --
MISINGI YA MAISHA YA FURAHA.
- Upendo
- Uadilifu
- Ushirikiano
- Unyenyekevu
- Uwajibikaji
- Ukarim n.k.
Natumai tumeenda sambamba vizuri mno
na hongera kwa kunifuatilia,endelea kuwa
karibu na wezamtima@... uzidi kuimalika.
Anthony Elia Mwak
Mwandishi
Muigizaji
Mjasiriamali
Wezamtima@gmail.com
www.wezamtima.com
Tel. +255659594226
+255738651846
Dar es salaam =Tanzania.
Kina cha fikra hakina ukomo.
No comments:
Post a Comment