FIKRA ZA DHAHANIA
Mwonekano wa maisha ya mtu
ya sasa -upo kama alilivyokuwa
akiwaza na kutenda mawazo-
hayo wakati uliopita.
Ubongo wa mwanadamu umebeba
maajabu mazito mno,ubongo ndiyo kiongo-
zi mkuu wa maisha ya mtu. Ubongo hushirikaiana na milango ya fahamu, moyo
,na viamshi vingine vya hisia kumpa mtu----
mwonekano halisi wa maisha.
Milango ya fahamu pua,masikio,macho,nk.-
hukusanya taarifa fupi na kuzipeleka katik
ubongo kupitia neva ili taarifa hizo zikataf--
Siriwe -na zikishatafsiriwa hurudishwa ktk
mwili ,pia ubongo huamulisha mwili ufanye kitendo kulingana na jinsi ulivyotaf-
siri taarifa.
Kwahiyo ukiangalia kwa kina utagundua---
kuwa kumbe mwili hufanya kazi kama hali-
mashauli,(yaani kwa ushirikiano wa ajabu),
ukiongozwa na ubongo.
Nachotaka ujue hapa ni kwamba, uwe mak-
ini sana ktk kuutumia ubongo kutafsiri taar
-ifa, maisha yako yatazid kuimalika zaidi ---
kama utafsiri taarifa nyingi ktk hali chanya
kuliko hasi.
Eneo hili ndio kiini cha maisha na ndipo --
tunapotofautiana kati ya binadamu mmoja
na mwingine.
Ktk dunia hii utakutana na taarifa za kila --
aina,nzuri na mbaya -lakini kama hautawe-
za kupembua ktk hali chanya ujue kuwa ni
lazima tu utakuwa mtumwa wa fikra zako.
Akili ina upana sana ktk kufikiria, ---lakini ktk fikra kuna fikra za dhahania na--
fikra za kawaida. Nadhani ulishawahi kuw-
aza vitu mpaka wewe mwenyewe ukawa --
hauna uhakika kama yatatimia uyawazayo.
- FIKRA ZA DHAHANIA .
Fikra za dhahania ni nini?
Fikra za dhahania ni mawazo ya --
kina yanayopambanua vitu visivyo oneka--
na, shikika wala kudhibitika.
Watu wengi wanateswa na fikra hizi wana-
waza maisha kwa kina kisichofikika na ku-
ona kama ni muuzija tu wengine kufaniki-
wa na wengine kuwa maskini kimaisha.
Kama unawaza vitu ambavyo hautaweza
kuwaelezea watu wengine hazarani bila ya
aibu ama uwoga - basi vitu hivyo havitatokea.
Maisha sio bahati,miujiza,wala nyota. Bali--
ni namna unavyongoza mwili na akili yako ambavyo tayari Mungu alikwisha viumba,
na wewe ndio deleva.
Mafanikio yoyote yanatoka ktk fikra sahihi zilizotokana na taarifa unazopokea,tafakari
na tengeneza mfumo wa maisha wa kawaida tu wala usiwaze sana ,ila kuwaza ni jambo jema sana.waza ktk hali chanya --
na tenda zaidi.
HASARA ZA FIKRA ZA DHAHANIA
- Utumwa wa fikra.
- Sononeko la moyo(mfadhaiko).
- Kukata tamaa.
- Ulemavu wa fikra.
- Kupoteza imani.
- Kulaumu watu.
- Upweke.
- Kutokutimiza ndoto.
HATUA ZA KUEPUKA FIKRA
ZA DHAHANIA
1. Kiasi.
Kuwa na kiasi kwa kila jambo unalofikiria
na kutenda.kutokuwa na kiasi hupelekea
ulevi na utumwa wa fikra.
2. Mfumo.
Weka mfumo wa maisha ukuongoze ,yaani
amua unaishi maisha ya aina gani na uyaishi kwa furaha bila kuvunja heria.
3.Vipaumbele.
Pangilia mambo yako na uyaweke ktk kuyatenda kulingana na umuhimu wake.
4.Ratiba.
Moja ya njia zinazowafanikisha watu ni--
kuwa na ratiba ya siku na kuifuata hiyo --
Ikuongoze kwa siku nzima.
5.kujitathimini.
Ukishakuwa na ratiba ya siku yako-
mwisho wa siku yako - kaa chini uitafakari siku yako ulivyoipeleka kulingana na ratiba
yako. Jitathimini na ujipongeze na ujirekebishe ulipokosea .
Sina la ziada mpezi mfuatiliaji wa makala haya ya WEZAMTIMA. Hongera sana kuwa nami na endelea kubadiri fikra
Ndani ya mgodi huu.
Anthony Elia Mwaka
Mwandishi-
Muigizaji
Mjasiriamali
Tel. +255659594226
+255738651846
Wezamtima@gmail.com
Website- www.wezamtima.com.
Dar es salaam - Tanzania.
Kina cha fikra hakina ukomo.