UPANA WA ELIMU.
Kila swali katika dunia hii,
linaweza kujibiwa kwa majibu-
matatu yenye maana tofauti-
kabisa.
Dunia inashangaza sana ,mpenzi mfuatiliaji wa blog hii, -hasa ukiangalia maajabu ambayo Muumba katuumba nayo katika akili zetu sisi wanadamu.
Huwa tunazaliwa tukiwa na akili changa na kuanza kufundinshwa na kujifunza hadi mwisho wa maisha yetu ya duniani. Kumbe suala la kujifunza na kufundishwa ni suala endelevu hadi mwisho wa muda wa mwanadamu hapa duniani.
Maarifa ni dimbwi la uchafu-
ambapo mchanganyiko wa huo
Uchafu,unaweza ukazalisha kitu -
kizuri sana kiitwacho Elimu.
Hauwezi ukawa na nidham ya hali ya juu sana ya kuogopa kutukana - kama hauyajui matusi yenyewe.
Hivyo basi maarifa huwa yamegawanyika, yaani mabaya na mazuri na kazi ya binadam ni kuchambua kipi anahitaji kukitenda maishani.
Ndugu yangu msomaji, mada yetu ni ndefu kidogo, hivyo najitahidi kuiweka kwa ufupi ili niguse kila kona ya ufahamu wako ipasavyo.
Nadhani ushawahi kukutana na maswali yakakuchanganya ,hasa namna watu tofauti walivyokujibu na kila mmoja kwa maana na majibu tofauti kabisa. Na ukawa unajiuliza sasa ni yupi au n jibu lipi litakuwa sahihi.
Hapa ndo linakuja suala la upana wa Elimu kwa ujumla wake ,kwamba kuwa -kila swali lina majibu matatu yenye maana tofauti kabisa .majibu haya hujikita katika vipengele vitatu tofauti -navyo ni:-
- Maarifa ya jumla ya dunia
- Maarifa ya uthibitisho wa imani
- Maarifa ya upeo binafsi.
Tuangalie mfano wa swali linavyojibiwa kwa hivyo vipengele vitatu juu.
Mfano. Kwanini maisha ni magumu?
Majibu.
=maarifa ya jumla ya Dunia.
Maisha ni magumu kwa sababu watu walio wengi wanaishi bila utaratibu wa kujua kanunu na siri za mafanikio .
= maarifa ya uthibitisho wa imani.
Maisha ni magumu kwa kuwa baada ya binadamu kuasi katika busitani ya Edeni -alifunkuzwa na kutupwa duniani na Mungu akamuamulu kuwa ataishi kwa jasho lake. (-kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako. Mwanzo 3:17-18).
=maarifa ya upeo binafsi.
Maisha ni magumu kwa sababu wanadamu hatuna nia ya dhati ya kusaidiana .
Nadhani umeona maarifa yalivyo gawanyika na umeanza kupata mwanga wa kusudi la mada yetu ya upana wa Elimu. Lakini nikwambie tu rafiki yangu kipenzi kwamba: maswali mengi watu hupenda kuyajibu kwa maarifa ya jumla ya dunia ,na mengine kwa maarifa ya uthibitisho wa imani, na ni Mara chache sana mtu kukujibu kwa maarifa ya upeo binafsi, na hapo ndo kwenye siri ya mafanikio ya mtu.
ELIMU NI NINI?.
Elimu ni mfumo wa mafunzo yanayopatikana shuleni,vyuoni na maisha ni.
Aina za Elimu - mfumo wa Dunia.
- Elimu ya msingi
- Elimu ya sekondari
- Elimu ya vyuoni.
MAARIFA NI NINI?
Maarifa ni njia inayotumika kujitoa katika shida ama kuweza kupata kitu. Maarifa ni Elimu au ujuzi.
Aina za maarifa katika Dunia.
- Maarifa mazuri
- Maarifa mabaya.
-wazazi wanapaswa kuwafundisha-
watoto wao namna ya kutafuta maarifa.
Na sio tu inatosha kusisitiza watoto-
wasimwache elimu aende zake.
Kazi ya Elimu katika maisha ya binadamu.
- Kumlinda mwanadamu.
- Kumwezesha apate anachokitaka.
- Kutambua uwezo wa kipekee alionao.
- Kumsaidia kutatua shida zinazomkabili.
- Kurahisha maisha.
Kwanini wakati mwingine Elimu haiwasaidii walio nayo.
- Ni namna tofauti walivyoipokea Elimu.
- Nidhamu ndogo ya kuiishi Elimu waliyo nayo
- Imani hafifu. Wengine wanaamini elimu walionayo ndo inafaa tu na ndo ya mwisho.
- Mufumo wa elimu usiokidhi peo za kimataifa za kujitambua,kujitegemea na kujiajiri.
Chakufanya ili kuwa na Uhuru
wa Elimu na maarifa.
1. Kujitambua. Kujua maana ya Elimu, kuwa tunasoma ili kuongeza na kukuza peo zetu ili kurahisisha utatuaji wa changamoto zitakazotukabili.
2. Imani.kujiamini na kuamini uwezo wako wa ndani na kuendelea kuukuza kwa kujifunza na kutenda.
3.mahusiano.Maarifa mazuri ni yale yanayonuai kuifanya dunia kuwa sehemu nzuri ya kuishi .
4. Ndoto/ malengo
5. Kujifunza.namna bora ya kufika kunako ndoto zako.
6. Anza sasa thubutu.
Kinachomtofautisha mtu-
mmoja na mwingine -sio akili au-
bahati ya kuzaliwa.Bali ni mapokeo
na matunizi ya Elimu na-
Maarifa mbalimbali.
Nakushukuru kwa kufuatana nami hadi tamati ya mada yetu ,natumai umepata mwangaza mpya wa namna ya kuishi . karibu na endelea kufuatilia wezamtima@.. Kina cha fikra za utafiti na uzoefu wa maisha.
Anthony Mwaka.
Mwandishi.
Mujasiliamali.
Muuigizaji.
Tel: +255738651846.
+255659594226.
+255659594226.
Wezamtima@gmail.com.
Kina cha fikra hakina ukomo.